UTENZI WA KIYAMA, 1 # Akhi nipatia wino na karatasi mfano na kalamu muawano ilonjema lcwandikia* 2 Unipatie mahali nikae nitajamali nitunge yangu akili niwaze nikishangaa, 3 Kandike Jina la Mungu Bismi lahi wa taMgu mwenyilcutandika mbingu na nchi zikatangaa. 4 Kandike na Rahamani mueneza duniani kwa viumbe na majini na nyama wakutambaa* Hiandike na Rahimu muwaruzuku hirimu na wavele wa kadimu na wake wasiozaa. 6 Kupenda kwake khalaki wote huwapa riziki hasahau makhaluki ambae hakumjua* 7. Hapa nilipokomele sihitaji kwenda mbele kwa sifaze mtaule Muhammadi mfadhwaa. 8 Sifa zake ni kathiri huzidi kama bahari siwezi kuzikadiri na kidhabtmi kungia. 9. Sifaze tutaziwata niwape niliyopata penyi ohuo hatafuta haiona hadithia. 10. Pana hadithi ehuoni ikanitiya huzuni vitukovye Rahamani alivyotuhadithia. 11 Hisoma sana kitabu penye habari ajabu yandishiwe kiarabu hisoma ikinelea. 12. Penye hadithi kitoto kina maneno mazito klna na swifa za moto nami tawahadithia. 13. Penye hadithi adhwima dunia itapokoma hiyo siku ya Kiyama kitakapo fikilia. 14. Mwanzo wake fahamuni atakapo Rahamani kuyondoa Buniani awalie tawambia. 13 Alisema Abdallah bin Abasi Fadkwila radhiyallahu taala kauli alipokea. 16. Alipokea kauli na Muhammadi rasuli swala llahu alaihim wasalama tasilima. 17. Alisema Muungama swala llahu wasalama hiyo siku ya Kiyama kitakapo tookea. 1 8. Atae kuwapo nani kwa miaka arubaini pasi ia ji visimani vyote vitakaukia. 13. Pasi riziki ya kula wala usiku kulala wala kwenenda mahala kwa kifukuto kwingia. 20. Pasi kusema kukicha kwa kifukuto na shaka pasi nyama wa kuvuka kwa shida kuu na njaa,