UTENZI WA KIYAMA. BISUMILLAHI RAHAMANI RAHIMI 1. Yakhi nipatiya wino na kwaratwasi mufano na kalamu muawano ilokyema kwandikiya. 2. Munipatiye mahali nikale nitajamali nitunge yangu 'akwili niwaze nikishangaa. 3. Nanze jina la Mungu Bisum' Allahi wa tangu mwinyi kutandika mbingu na iti zikatangaa. 4. Nandike na Rahamani Muweneza duniyani kwa viwumbe na majini na nyama wakatambaa. 5. Niandike na Rahimu aruzukuye harimu na wavyele wakadimu na wake wasiwozaa. 6. Kipendo kyakwe Khallaki wote huwapa riziki hasaliyi makhuluki ambaye hakumujuwa. 7. 8. Hapo nilipo komile sihitaji kwenda mbele kwa swifa ya Mutewule Muhammadi Mufadhwaa. Swifaze haziwezeki wala haziwangiki ni laki laki lukuki punde kuzidiya. 9. Swifa zakwe ni kathiri huzidi kwamba bahari siwezi kuzikwadiri nacha dhwabini kungiya. 10. Swifaze tutaziyata niwape nilizo pata penye kyuwo khatafuwata khaylowona hadithiya. : 11.......