Citation
Poems by Aziz bin Abdallah (MS 380446a)

Material Information

Title:
Poems by Aziz bin Abdallah (MS 380446a)
Series Title:
Miscellaneous Swahili manuscripts :
Creator:
Aziz bin Abdallah ( Author, Primary )
Publication Date:
Language:
Swahili
Materials:
Paper ( medium )
Technique:
Typescript manuscript Typescript with black ink on white pages; two pages are respectively yellow and green. All material is contained in a brown open folder within a white envelope

Subjects

Subjects / Keywords:
Swahili poetry ( LCSH )
Kiswahili mashairi
Genre:
Poem
Shairi
Poetry ( LCTGM )
Shayari
Spatial Coverage:
Africa -- Kenya -- Mombasa County -- Eastern Africa -- Mombasa
Coordinates:
-4.05466 x 39.66359

Notes

Abstract:
This MS contains a small collection of short poems by Aziz bin Abdallah ‘Kiwillo’, from Mombasa, dated between 1962 and 1972. The list of poems is as follow: - Sabasi na Siri - Cha Kutu - Mtwaa Wengi Pamoja - Mtu na Tabia Yake - Mgeni Karibu Chai - Wezi - Mwito - Wakeliko Wanawali - Ganda aina Gani? - Lijalo Kuja Kupata - Kula Mbili Moja Weka - Muiza Kondo - Mdigo - Keki - Bibie na Kusia - Nilipi Ulilo Taka? The poems are written in modern KiMvita, which is easily readable, with some influences of KiMrima, southern dialect. The poems discuss various issues of popular Swahili culture. For instance, “Mgeni Karibu Chai” tells of a guest (mgeni) in a household who is given tea (chai) and eggs (mayai), which will give him strength. It also provides information about the properties of tea and how it is made. Or, “Mtu na Tabia yake” tells of the different types of human characters and personalities. And, finally, “ Kula Mbili Moja Weka” advises that those in receipt of a salary should always set a sum aside in case of problems or loss of job. ( en )
General Note:
Biographical information: The author is a known poet from Mombasa who provided J Knappert with poems and information on Swahili poetry.
General Note:
Date of Composition: 1962-1972 AD (1382-1392 A.H.)
General Note:
Languages: Swahili (Roman script)
General Note:
Dialects: KiMvita
General Note:
Poetic Form: Shairi
General Note:
Extent: 15 leaves
General Note:
Incipit: Sabasi na Siri. Kumpa siri sabasi, ujuwe uta juponza,
General Note:
Archival history: Gift via Dr. J. Knappert from author, Aziz bin Abdallah, 1 May 1987
General Note:
Africa -- Eastern Africa -- Kenya -- Mombasa County -- Mombasa
General Note:
Gift via Dr. J. Knappert from author, Aziz bin Abdallah, 1 May 1987

Record Information

Source Institution:
SOAS University of London
Holding Location:
Archives and Special Collections
Rights Management:
This item is believed to be in the public domain
Resource Identifier:
MS 380446 ( SOAS manuscript number )
MS 380446a ( SOAS manuscript number )

Downloads

This item has the following downloads:


Full Text
* SABASI NA S I R I*

Kumpa siri sabas^i, ujuwejata
Itakuwa ni wepesi* kha"bari kaieneza*
Hataweza kujl kisi moyoni kuji kataza,
Kumpa siri saS'asi, wa^mtuma kutangaza*

Sabasi ni yake jinslf fyawatu kuyatangaza,
Iwapo uta-iauhisi, uwogope kumjuza,
Msije let a utesi* kotini mka ^ikweza,
Kumpa siri sabasi* wsumtuma kutangaza*

Hodari wa kudadisi ya watu kupeleleza,
Apatapo enda kasi, kwa nyonda kumdojteza,
Uli mwambia kiyasif yeye mangi w"Eaohgezaf
Kumpa siri sabasu wa mtuma kutangaza*

Aziz Bin Abdallah

MOMB ASA

5/6/72 *


Chakutu

Muhibu mwana mjomba, hu d a pigwa na dunia,
Sikae ukijigamba, maringo kutu tiliaf
Hayo usirige ya lumba, hovyo kuji ropokea,
Atumiyae cha kutu f lni kwamba kizima hana,

Y^le unae muwona, cha kutu yuwa tumia,
KtMbnka kizima liana, hajuwi pa kupatia,
Shida inapo kubana, s ighalabu kutagua, ^hUcAr^
Atumiyae cha kutu, ni IwamBa kizima hana#

Wewe cha kutu hutaki, sababu yake twa 3uaf
Kwamba huja pata dhikif ndipo uka kikataa,
Maneno ya miaJPlkl, usiwe uta twambia,
Atumiyae cha kutu ni kwamba kizima hana*

VVengi walio jisifu, na mno ku^ishaua,
Kujipa ukamilifu, mfano wake JalTa,
Kwa sasa ni wasumbu3Puf vibaya wavitapia,
Atumi^ae cha ku^u^ ni kwamba kizima Eana

Sema na kutafatori na moyo kujiutia,
Leo unacho kizuri, kesho kina kupotea,
Wabaki ^tahayarif waomba wa pita ndiaf
Atumiyae cha Taitu ni kwamba kizima hana*

Tamati nilipo fika, kalamu na watilia,

Kwako niliyo tamka, machache ya kutoshea,

Haya usipo ridhika, mengine takuletea,

Atumiyae cha kutu, ni kwamba kizima hana*

Aziz Bin Abdalah,

MOMBASA

27/8/69


1 MTWAA MENGI PAMOJA

Mengi unapo yasoza, na yote ukayataka,
Pasi ya mwanzo kuwaza, ni vipi uta yashika
Mengine hut a ya?/eza, huwenda kuku pony oka,
Mtwaa mengi pamoja, mengine humponyoka*

Uyashikapo kwa pupa, kwa saa au dakika,
Mengine uta yatupa, tini nayo kuanguka,
Kana urad shika tupa, utaona ya vundika ,
Mtwaa mengi pamoja, mengine humponyoka

Unapo ya twaa mengi, ili upate sifika,
Kwa wachache au wengi f watakuwa wakuteka,
Waseme mvita bangi, akili zime mmika,
Mtwaa mengi paraoja, mengine humponyoka*

Muole Mola Karinru, bwana ale takasika,
Kazi zake zamuhimu, kagawa kwa malaika,
/akae kuzi hudurnu, hadi kiyama kufika,
' twaa mengi^pamoja, mengine humpony oka#

Yuko atowae juwa, mtana kutwa kuwaka,
Yuko mnyesha mirnwa, na riziki kadhaiika,
Na yuko anae uwa, ni ziraili kumbuka^
Mtwaa mengi pamoja, mengine humponyoka*

,/engine wana tawala, nyota ziso hisabika,
vVengine washika swala, wa mswalia Rabuka,
Kutwa kucha pasi lala* hawasemi wana ehoka
Mtwaa mengi pamoja, mengine humponyoka*

Leo vipi mja wewe, kujitia madaraka,
Mambo yote utukuwe, huwezi kuyapeleka,
Kheri sasa uyagawe, tena basi kwa iiaraka*
Mtv/aa mengi parrtoja, mengine humponyoka*

Hili limeslia kushinda* kweli hutaki tamka,
Mbele haliwezi kwenda, huku nyuma kuondoka
Lime baki kusaranda, kila tuki limwilika,
Mtwaa mengi pamoja, mengine humponyoka*


MTU NA TABIA YAKE

1 Mola ale mjalia,kwa lie tabia yakef
Ndiyo anayo tumiafkatika maisfaa yakeg,
Sineni yawe udhia^kmsibu kumbu mtambuke 9
Jina nimoja lawatUg, tabia mtu nsyaka*

2* Wengine watumia* tabia ya usalata*

Mwawenzao huwingia fyawatu kuyatafuta*
Yakwako ukipw^M*,mwengiBe ataipataf
Jina nimoja lawatu*tabia mtu nayake

3* Wengine wana tumia*tabia ya uhasidi*
Kijito liuku fanyia^upawaoho na Wadudl^
Lam uki muaehiatliukifaai?ibu kusudlf
Jina nimoja lawatuftabia mtu n&yake*

4* Wengine wanatumia^tabia kusengenyamaf
Kutwa hawesi tuliafmwengine kmt mnenaf
Japo ila }ramtia*yoyote iso maanaf
Jina nimoja lavatuftabia mtu nayake*

5* Wengine wanatumiaf tabia ya mfedhmli*
Akfaeri ukimpia^liaitlki kwa jamalig*
Huwa aku singiliafakuwna bapadh,ulif
Jina nimoja lawatuftabia mtu nayake*

6* Wengine wanatmmiaftabia ya udhalimu^
Husimama J^enye ndiafakisubisi kaumut
Wensiwe kuwavi^ia^lra wanyamgfanya ddarahimuf
Jina nimoja lawatu^tabia mtu nayake*

Wengine wama tumia^tabia yamnafiki^
Yake uki yasikla^usemi faauna hakif
Haneni lenye sfaepia^moja likakuwafikif
Jina nimoja lawatu*tabia mtu nayake*

B Wengine wana tumiaftabia yakunwa tembo*
tlmuwone kwenye ndia^nae enda kombokoiibf
Usip muangaliafbudi akupige kumbof
Jina nimoja l&watu,tabia mtu nayake

9m Wengine wana tumla,tabia ya kugombanat
Kisa huku tafutiafambacho sieha maanaf
Apate kukurukiatlli mupate pigana*
Jina nimoja lawatu*tabia mtu nayake*

10 Wengine wana tumia*tabia ya taratibu*
Popote ana tuliatatun^a yake adabu*
Huwa hapendl udhia*kujitia kwenye tabu,
J ina^nime|a_lawatu ^ tab ia mtu nayake^

11 Wengine wanatumiaf tabia ile^yapimdaf

Fimbo sipo mpigiafhuwa nashida yakwenda*
Tazameni ya dunia^mambo Tile yana kwendaf
Jina nimoja lawatu,tabia mtu nayake

129 Tamati naishilia*sfaairi liwe nibasi

Yakiwa yatatukia^majambo ya wasi-wali^
Tuna muomba Jalia^ayaepuslie upesi*
Jina nimoja lawatu,tabia mtu nayake*

Aziz Bin Abdallah,
MOMBASA.

29/8/62*


/

mgeni karibu chai

1# Mgeni karibu chai, na mikate ya mayai,
Kunwa nawe ufurai, upate kutanabai,
Anwae hakunguwai, na ndiyani hasang&l,

Mgenl ¥arTbu cHal, na mikate ya mafai#

2# Kunwa chai mpendeka, upate kumakinika,
Kwako khabari nataka, zakule unakotoka ?
Kitambo uliondoka, sasa karibu ya mwaka ,
Mgeni karibu chai, na mikate ya mayai*

3 Kunwa chai ya m&zlwa, kwetu ulo andaliwa,
Usiwate ika powaf hamu haita kutowa,
Ni kinywaji cha muruwa, mgeni kukirimiwa,
Mgeni karibu chai, na mikate ya mayai*

Chai kinwadi damala, mekutilia vanila,
Na mikate pia kula, mizuri isiyo ila,
Kunwa upate kulala, chai haina ^^kM^^o^

Mgeni karibu chai, na mikate ya mayai*

5* Ghai haina ubaya, mgeni nina kwambiya,
Kunwa us ione hay a, watu wote watuiaiya,
Sukari mekutiliyaf nimesha kukorogeya ,
Mgeni karibu chai, na mikate ya mayai*6* Chai ni kinwaji bora kilicho shinda

Hunwa walo masogoraf na watezaji mpira,
Kinwaji kiao hasara, kina ongeza buswara,

Mgeni karibu chai* na mikate ya mayai

7* Karibu chai mgeni, utokae safarini ,

Kinwaji chenye thamani chenye sifa duniyani,
Itumikayo nyumbani, kadhalika na kassini,
Mgeni karibu chai* na mikate ya mayai*

3 Kunwa uta tabasamu* moyo usi udhulumuf
Mie nime jilazimu^ y^XS^^^I^^WMM^^
Nili iyona itamu, ndipo nikak^karimu,
Mgeni karibu chai, na mikate ya mayai*

9* Chai kinwaji ariffu, ambacho hakina khofu,
Kilo jaa utukuFu, mfano wa masharifu,
Ni nzuri yake haruftt, na koapxa^IIaWi
Mgeni karibu chai, na mikate ya mayaTT

10* Mgeni shika kikombe tukinwa chai tuimbe ,
Tuimbe mwana wa ng*ombe, usitese nazo pembe,
^ g j*££g usile maembe, ulapo usijirambe,

"ffgeni karibu chai, na mikate ya mayai*

c

Aziz Bin Abdallah,

P. 0. BOX 90103,

M 0 m B A S A.
IS 15/5/72,


WeziHime kwisha fikiria, katika yangu nafusi,
Kila niki yapimia, hamna imani nasi,
Ndipo muka tufanyia, aawi kupita kiyasi,
Kila niki angalia, hamna imani nasi.

Shida zime tutatia, zinatupa wasi wasi,
Tuketipo tunalia, na kutokwa na kaaasi,
Mechoka kuvumilia, wenzetu aso jiklsx,
Kila niki angalia, hamna imani nasi.

Ya kweli tawaambia, japo taleta utesi,
Lau muta nivamia, nanyi kuja tonifosi, fafrftx.Yote^Mle yarldhia# munipige na risasi,
Kila niki ang&lia, hamna imani nasi.

Yanini kutukamia, na hali sisi kwa sisi,
Mazito kuromilia, sambe ni^ambo rahisi,
Baki twa watukulia, kuuwepuka jakosi,
Kila niki angalia, hamna imani nasi.

Imani raume susia, mwaiyona kitatusl,
MazurikutufSnyia, kwetu hali tuhalisi,
Macro awa tujazia, kana tulo na vis alii
Kila niki angalia, hamna imani nasi.

Bwana wetu wadunia, tunakuoraba Mkwasi,
Zigo ktttupu||gttziaf la ttmaiza tfiii ~
Duwa hil fikiria, n^eaa kana aliiasi ,
Kila niki angalia, hamna iaani nasi.

Wezi watupa udhia, daiaa wana tughasi,
Madiaka wa tuvundia wakitukuwa wOammtp f u* "
Aidha na pes a pia, na nguwo zetu libasi,
Kila niki angalia, hamna imani nasi.

Taaati na ishilia, kutunga hapa nibasi,
Mwito wako twaridhia, Mpenzi wetu Haisi,
Tuko iaara raia, kusaidia Polisi,
Kila Aiki angalia, haiana imani nasi.Aziz Bin Abdalla.


MWITO

Mtu hakatai mwito, ilawako na ukumba,
Mwito wako wakitoto, hatmipasii kwa^ba,
Tena ndani unakoto, usi^e uka. nitixaba,
Mtu hakatai mwito, ila wako siutakiV

Waniitia mazito, nami "bado ni mtamba,
Ndipo nikafanya sito, nakacha mfano tumba,
Na kutizama kwa mato, sina nguvu za msamba,
Mtu hakatai mwito, ila wako iiutaki.,

Mwito wako siwapato, nije uwombe yigamba,
Kukupa naona 3oto, utanitia ukomba,
Kwa mana na kujuwato, wewe mtu wa kupemTDa,
Mtu hakatai mwito, ila wako siutaki*

Nime^ifanya masita, sisikii ukinamba,
Jitafutie maplto, unapebeba mtumba,
Mie sitaki sakato, wewe kwangu huiia rimba,
Mtu hakatai^mwllio, ila wako siutakiT^""

Nilo nena uwazeto, ewe mlaji maramba,
Au nexida kauzelTo, siyapendi ya TSTtimba,
Sinitie mkengVeto, nikabakia kusumba,
Mtu hakatai mwito, ila wako siutaki

Moyo una ms&fc&to, ni kuonapo huvimba,

Lau nashika Ifigoto, takupiga kana simba,
Wala sifanyi iafu^Eo, ya kweli kwako naamba,
Mtu hakatai mwito, ila wako siutaki.

Tamati kilo cha mboto# sikupi mwana mjomba,
Hat a nikala mghe^oj sikwambii nawe ramba,
Sikupi hata kipeto, kwa kukaona wamba,
Mtu hakatal otITo, ila wako siutakiAziz Bin Abdallah,

M 0 MBA S A

12/6/72

ON JL33HS

axva

ON

oj- wvvivs sh yva -an od i a s


1 Wakeliko wanawali

Editori tafadhali, na kuomba kwalsani,
Pokea shairi hiJLi, ulichape gazetini,
Litoke mwezi wapili, likasomwe na jirani,
Wakeliko wanawali f humu humu majumbani,

2. Maneno yako sikweli, ulo sema Ramadhani,
Yakuhusu wanawali,' wamekwisha majumbani,
Mimi'hayo sikubali, wala haiwezekani,

Wakeliko wanawali, humu humu majumbani.

3. Nakupa hii mithali, isikize kwa makini,
Kila palipo katili, huwako mwenye imani,
Kilieho anza azali, leo hakikosekani,

Wakeliko wanawall, humu humu majumbani.

4 o Juzi juzi Jfujnapili, kaowa "bwana Hasani,

Aliowa mv/anamwali, akaingia nyumbani, i /
A1 imp a ta^aii 1 i, mke wake harusini, f^^

^ WaTeTIko wanawali, humu humu majumbani. ^ ^ r'J!

b. Wale waso ikibali,( wazururao ndiyani,

Sivyema loawa kejeli, na kuwatowa thamani,
Maisha ya zadnKaTx*/ ya mwelea Rahamani,
Wakeliko wanawali, humu humu majumbani

6o Mola kaumba mawili, kwetu sie ubaini,

Ni subili na asali, utaulie rohoni, N

Mwenye mehgi na akali, siri yake imbinguni, r

Wakeliko wanawaliTaumu humu majumbani.

7. Wazee kupenda mali, hawajawa makosani,
Mali ni pepo yafpxli, kwa walio duniyani,
Maisha yenye thakili, aya pendae ni nani?,

Wakeliko wanawali, humu humu majumbani*

8. Wasicrjali muhali, wakawamo fedhehani,
Siwote wenye naftiili, wako walo sitarani,
Kama siwewe ni'Ali, humo humo mitaani,

Wakeliko wanawali, humu humu majumbani.

9 Nyumba ialo zikabili, kuchunguza walo ndani,
Hilo s^ijambo jamali, >

Kesho Abele ya Jalali, utakwenda sema nini?,
Wakeliko wanawali, humu humu ma$umbani.

10 Tamati ya wanawaii, nayo isibwage.......zani,

Ukijifanya wakili, nijie vyema kotini,
Lakini usi badili, kisa hiki muhisani,
Wakeliko wanawali, humu humu majumbani.

Aziz Abdallah Kiwillo,

B. 0. BOX 90103,

M 0 M B A S A,GANDA AINA GANI

Chama hichi Amkeni, kilicho huku Iwandoni ,
Kwa leo kime taSaiii, kuwauliza jamanf
Higanda aina gani, lilo m?bwaga fulani ,
Nasitwataka tujuwe, niganda aina gani?

(Janda hilo twasikia, linapo imbwa ngomani,
Bado twali fikiria, na hatujalibaini,
Ndugu mnapo twambia, tutakuwa fufaEani,
Nasi twataka tujuwe, niganda aina gani?*

Hilo niganda la ndizi, au ni latunda gani?
Twambiyeni wazi-wazi, wala msitufiteni,
Ime tujaa simanzi, kukosa kulibaini,
Nasi twataka tujuwe, niganda aina gani?

Kiwa niganda JLafembe, nanyi ndugu twambiyeni,
Nasi piya tuliimbe, tukiwako tarabuni,
Hatutahofu viumbe, wakitaka ushindani,
Nasi twataka tujuwe, niganda aina gani?

Nauliza nisejuwa, mnitowe ujingani ,
Kiwa niganda la muwa, au nila kudlumajir,
Ubora nikuambiwa, nitiiawabu dimiyani,^
Nasi twataka tu,juwe, niganda aina gani?

jl o (n^ ^ Cf

Japo mlitaja ganda,
Eadiri tunavyo penda
Nasi tupate jilinda,
Nasi twataka tujuwe,

Si kwamba twakusudia
Hiyo siyetu twabia,
Kwenu tume swafinia,
Nasi twataka tujuwe,

lilikuwa ganda gani f
aina yake tajeni?
tulionapo ndiyani,
niganda aina gani?

kuwatafuta undani,
vijana wa Amkeni,
twaapa kwa Rahamani,
niganda aina gani?

Kiwa niganda lAuyu, nanyi tuelezeeni,
Aula nila papaya, nanyi tufahamisheni ,
lasikini mtu huyu, twamuonea imani,
Nasi twataka tujuwe, niganda aina gani?

Nihino yetukhabari,
Wala hatutaki shari,
Jawabu twa isubiri,
Nasi twataka tujuwe,

hapa twa*-f unga unenif
na tumlani shetwani,
ijapo pindi mwakani,
niganda aina gaxii?

Aziz Abdallan Kiwillo,
P. 0. BOX 90103 f
MO M B A S A


' LIJALO KUJA KUPATA *Na kwambia mwana kwetu, maneno ya kutakata,
Wajifanya mtukutu, na kapenda vuta-vuta,
Na kuwadharau watu f yaja kufika mat at a,
Lijalo kuja kupata, usije uka niita*

Like nyuraa lile janga, kwako lina jikokota*
Lijapo lika kuzonga, juwa halita kuwata,
Utarusha lako pangaf kitu liehindwe kukata,
Lijalo kuja kupataf usije uka niita*

Mimi sasa simwenzako, na ichelea aakata,
Siwezt msuko suko* wala siwezi kuteta,
Mbali kwani nitokako, mengi nilio yakuta,
Lijalo kuja kupata, usije uka niita#

Kila apendae siiarif sitaki kumu ambata*
Shari sikitu kizuri, mtu kwenda itafuta,
Mbeleni ina khatwari* mja huja kuyapataf
Lijalo kuja kupataf usije uka niita

engi nilio ?/aona, zama walio jikita*
Leo wame tulizana, wame bakia kujuta*
Hawana tena namna* wabaki teza karatat
Lijalo kuja kupata* usije uka niita*

Usije aema mwenzangu* yakuwa nime kuwata,
Ujapo pigwa marungu, usaxabe nita kufwata*
Nitabaki kwenda zanguf kiehakani kujifita,
Lijapo kuja kupata, usije uka niita*

Juzi juzi mwafulani9 akiringa na kunyetaf
Alitiwa msowani, bila yakufurukuta*
Akawa hali tabani, kabaki kuji kunyata,
Lijalo kuja kupata, usije uka niita*

Na umaliza usemif na kai&tasi na wataf
Sije nikalia yomif nisijuwe pakupita,
Kuja ambiwa ni mimi, hilo halitanipata,
Lijalo kuja kupataf usije uka niita#

Aziz Abdallah KiwilloMombasa

5/10/7;'KOLA MBILI MOJA WEKA

Aziz Amallah Kiwillo

p. 0. box 90103


MUIZA KONDO

Muhibu na kueleza, nikwambiayo kamata,
Sikae ukitangaza, maneno ya asalata*
Mwishowe yaja kup&za, uselehe lot juta,
Muiza kondo us ambe, kuwa ha*vezi" kateta*

Usambe muiza kondo, kuwa Iiawezi kuteta,
Kwafimbo aula nyundo, yuwaweza kukugota,
Akakufunga mafundOj usiweze kuyakata,
Muiza kondousambe, kuwa hawezi kuteta.

Usione katulia, nae ame jikunyata,
Ikawa wamtezea,ushari Eiimtaf^
Juwa akikuvamia, kwake hutaf^ixnikuta,
Muiza kondo usambe, kuwa fiawezi kuteta*

Ameona siuzuri, wewe nae fek&t&ta,

Ndipo akawa shwarl., samanani ukapata,

Basi ujitahadhari, usiyalete matata,
:ruiza kondo usambe, kuwa hawezi kuteta*

Tamati kadi watama, yakweli sit a kufiia,
Utajitia kilema, kipiga ngumi ukuta,
Niheri urudi nyuma, kondo siyakuifwata,
Huiza kondo usambe, kuwa hav^ezi kuteata

1 M D I G 0 1

Hataka kuwauliza, wazee hadi vijana,
.. ineno la kutukiza, wala sila kutukana,
Ajuwae kuneleza, anipe yake maana ,
Alikosani mdigo, hata kuitwa mzigo?*

Alikosani mdigo, hata wengi wakanena,
Mdigo kuwa mzigo, wala oso wezekana,
Akuoneshapo jego, tuseme hukutafuna,?
Alikosani mdigo, hata kuitwa mzigo?*

Neno hili hufikiri, nikawa furaha sina,
Laserawa kwa ujeuri, au kwa kutaniyana,
Nipeni ilo dhahiri, wala sio leaf it ana,?
Alikosani mdigo, hata kuitwa mzigo?*

Niyupi ata nambia, mdigo walibebana,
Akawa amlemea,kwa marefu na mapana,
Mwishowe aka mtua, akawa hanae tena,?
Alikosani indigo, hata kuitwa mzigo?*

Someni shairi langu,mabibi na kina bwana
Jawabu yenye matungu, siwe tuta ambizana
Naogopa bwana Mungu, sije akatupa lana,
Alikosani mdigo, hata kuitwa mzigo?.

Aziz Bin Abdallah

9

M 0 M B A S A

19/8/69


KEK I

lo Na mshukuru Karimu Bv/ana alia mbinguni,

Kuumba bina adamu wakawamo duniyani,
Na vyakiila vilo tamu, vya kutia. pumbazoni,
Duniyani kitu tamu, sijaona kama keki.

20 Keki chakula ajabu, mfano wake siyoni,

Hunyima wako B.wahibu f na ndugu wa matumboni n
Haswa iwe na zabibu, pamoja mdallasini,
Duniyani kitu tamu9 sijaona kama keki.

3 o Keki haina mithaii, utamu wake jamanip

Ime ishinda asalT, ladha yake ulimini,
Huku badili akili, tamu yake mdomoni,
Duniyani kitu tamu, sijaona kama keki.

4. Keki huku burnidisha, kiwa watoka kazini,
Muhibu akikulisha, hudhani uko peponi,

, Husahau kuswalisha, imamu msikitirii,

Duniyani kitu tamu, sTjaona kama keki.

5. Keki unapo iyona, budi utaitamani,
Ufanyiwapo hiyana, mwenzio akikuhini,
Moyoni uta 'sonona, ikupate na huzunl,

Duniyani"kitu tamuy sijaona kama keki.

60 Keki rahaye uaiku, au saa zajioni,

Pawe na nyama ya kuku, na maziwa gilasini,
Hunena kama kasuku aliyoko kitunduni,
Duniyani kitu tamu, sijaona kama keki.

^ Keki yashinda fal(*Ia? ladha yake ikhiwani, ^

Utaila ki maadjf, ikxwamo sahanini, (j

Husahat/yako shida, ulo nayo duniyani,
Duniyani kitu tamu, sijaona kama keki.

80 Keki ikole sukari, iive vyema jikoni,

Huta TEala lmsiibiri, uki iyona matoni,
Taitafuna kwa rnori, kana ule na shetwani,
Duniyani kitu tamu, sijaona kama keki.

9o Keki inayo pendeza, nn/hino muibaini,

Upate ya kuteleza, teha iliyo laihi,
Ndiyo ita kupumbaza, na kuila kwa makini,
Duniyani kitu tamu, sijaona kama keki.

10. Keki uwilapo mbivu, ikisha shuka tumboni,
Hujiona mlegevu, hakika mwako mwilini,

Uwi lap o _k_ YUYiivu ^t a j i ona t aaban i,

Duniyani kitu tamu, si;) a ona kama keki.

11. Keki ha-lkinaishi, uwilapo waswitani,

Wala hal.....TracEokeshi, kuitaftma menoni,

Haswa itiwe marashi. ya mti wa ^mrJLJiaiii,,

Dimly an i k i tu t amu, sija ona Team a keki.*

t ^ 12o Keki ni kitu jamala, tena ilo na thamani,
Urxapo taka kuila, stater uweko chumbani,
Tena upate mahala, ambapo ni faraghani,*
Duniyani kitu tamu, sijaona kama keki.

13 o Keki chakula na.......dhifu, itiwe iliki ndani, : ;

Wallahi yake harufu, haikukeri puwani, c^v, j.

- Japo ohilingi elifu, kununuwa hutamani,

Duniyani kitu tamu, sijaona kama keki.

Aziz Abdallah Kiwillo,


'BIBIE NA KUSIA*Kila siku mbili shika, sitano za mara rnoja,
Tano zinapo ondokaf zikenda hukawa kuja,
Zikija ume dMfika, kama debe la kuvuja,
Masikini akupae, sitajiri asokupa*

Japo wa mpenda lodi, kwa kuwona ana pesa,
Mambo mengi hufaidi, kwake yeye wayakosa,
Wa uvundaje mradi, kwa akupae sambusa?,
Masikini akupaef sitajiri asokupa*

Masikini akupae, ndie huyo kwako bora,
Yataka ukae nae, usifanye masikhara,
Yule akutizamae, kwake sizinge duwara,
Masikini akupae, sitajiri asokupa*

Tajiri ni wamwenziyo, ingawaje wamtaka,
Mapenzi uliyo nayo, kwake ukiyapeleka,
Enda kufukuza mbiyo, na izara kukufika,
Masikini akupae, sitajiri asokupa*

Masikini kwa hakika, uw^lewe akupenda,
Kwako ame swalitika, juyako amekonda,

Akukoa^^naijOka, huwa mfifana wang1 onda f
Masikini akupae, sitaji'ri asokupa*

Tajiri kwako h&simMs na wala hakutft^iaini,
Aona una wazimu, unga mpenda mqyonl*
Kukupa chake vigumuf shilingi aula peni*
Masikini akupae, sitajiri asokupa*

Masikini ndiye wako, anae kmxemmesh^9
Abebae tabu zakof pasipo kumohokesha,
Atunza maisha yakof chakula na kukuvisha,
Masikini akupae, sitajiri asokupa.

Tajiri anae wake, ampendae yakini,
Hataki kwake ufike, asubuhi na jiyoni,
Jituze u§p&lalka* nafukarao nyumbani,
Masikini akupae, sltajirFasokupa*

Masikini sihiyana, utakacho hakuhini,
Japo kiwe mbali sana, hukuletea mwandani,
Ukishikwa shikamana ,us iwe gu^kushani,
Masikini akupae, sitajiri asokupa*

Bibie wasia soma^niliyo kuandikia,
Yangu kwako nilosema, nawe kuyazingatia,
Nahapa naweka tama* yatoaha nilo kwambia,
Masikini akupaef sitajiri asokupa*

Aziz Bin AbdallahMOMBASA

12/5/72


nilipi ulilo taka?

1* Bibie nime kuweka, kwa wema nakwangalia,
Tangu ulipo olekaf nyumba yangu kuingia,
Niwezacho ukitaka, huwa nakutimizia,
Nilipi ulilo taka, kiwa sikukufanyia?.

2 Kukicha na -hangaika, chakula na kutumia,
Hukuletea kupika, wawili tukajilia,
Ulapo ukateuka, mda ukijishibia,
Nilipi ulllo taka, kiwa sikukuf anyia?*

3* Ngpwo nazo kadhalika, nyonda huku nunulia,
Sikila mwezi nimwaka, lakini na kukatia,
Wala sio zavirdka, mpya ukijivalia,
Nilipi ulilo taka, kiwa sikukufanyia?*

4* Maradhi ya kilpxshika, dawa na kutafutia,
Furaha huniepuka, kiwa waniugulia,
Tabu zako nptmashaka, mimi nazisimamli,,
Nilipi ulilo taka, kiwa sikuloifanyia? *

5* Jambo kwenu likizuka, msada na kutilia,

Kitakwacho liupeleka, mwenzangu kgtea£idia,
Wakwenu sije udhika, mawi waka simuTia,
Nilipi ulilo-taka^ kiwa sikukufanyia?#

6* Harusini ukitaka, kwenda sija kuzuia,
Usemapo naridhika, huwa nakukubalia,
Wakesha ukizunguka, pasipo kuku.fwatia,
Trillpi ulilo taka, kiwa sikukuf anyia?*

7* Sina siku nilitoka, kona nikakulalia,
Maasi nime epuka, nisi^khalifu sheria,
Ngfeala huja nishika, kuwa menifumania,
Nilipi ulilo taka, kiwa sikukiiTanyia?^

8* Vipi tena muhibaka, umebadili tabia?,

Mara huwa watoroka? nyumbani wanikimbia?,
Ukenda unako taka, pasipo na kunambia,
Nilipi ulilo taka, kiwa sikukuf anyia?*

9* Kama kwangu umechoka, sasa umenitukia,
Ukweli ni kutamka, penzi lime kuishia,
Wengi walio zalika, mwengine tajipatia,
Nilipi ulilo taka, kiwa sikukufanyia?*

10* Tamati nipe hakika, yale ulo*imsudia,
Kama wataka taj^fi, sema takuandikia,
Uwende unako ^Ika, kwani ni kubwa dunia,

Nilipi ulilo taka,' kilra sikukuf anyia?*

Aziz Bin Abdallah,

MOMBASA*

4/5/72 *


Full Text