Citation
Waadhi wa Sh. Abdalla al-Husniy (MS 380766a)

Material Information

Title:
Waadhi wa Sh. Abdalla al-Husniy (MS 380766a)
Series Title:
Yahya Ali Omar Collection
Added title page title:
Waadhi wa Abdallah al-Husni
Creator:
Al-Husniy, Abdalla, Sheik
Publication Date:
Language:
Swahili
Materials:
Paper ( medium )

Subjects

Subjects / Keywords:
Islam
Swahili poetry
Religious beliefs
Uislamu
Kiswahili mashairi
Imani za kidini
Genre:
Poetry (Shairi)
Shairi (poetic form)
Spatial Coverage:
Africa -- Kenya -- Mombasa -- Mombasa
Coordinates:
-4.05 x 39.666667

Notes

General Note:
First lines of manuscript: Bismillahi naanza jina la Mola muweza nipate kuyatimiza haya nalokusudiya
General Note:
Mistari ya kwanza ya hati: Bismillahi naanza jina la Mola muweza nipate kuyatimiza haya nalokusudiya
General Note:
Manuscript dates from circa 1948 A.D. (Gregorian calendar) = circa 1368 A.H. (Hijri calendar)
General Note:
Composition dates from circa 1948 A.D. (Gregorian calendar) = circa 1368 A.H. (Hijri calendar).
General Note:
Swahili text inscribed in Latin script (Romanised)
General Note:
Biographical history: Sh. Abdalla al-Husniy was born in Mombasa at the beginning of 1900 in a family that originated from Hadramaut. He studied Islamic teaching with Sh. Said bin Ahmed, a well-known religious scholar. Sh. Abdalla became a Sheikh at the Anisa Mosque where he tought for many years and where he was buried in 1955. He was known for organising the Maulidi celebration, in the Anisa mosque, that was attended by many people from the Coast. After the maulidi he used to composed his famous waadhi, of which this one is an example. Sh. Abdalla was Yahya Ali Omar's religious teacher.
General Note:
Archival history: Donated by Yahya Ali Omar in 2003
General Note:
Physical characteristics: typescript in black ink
General Note:
Relevant publications: P.J.L Frankl & Yahya Ali Omar. 19..Mashairi ya Waadhi. in AAP-Swahili Forum, Koln, Germany.
General Note:
Scope and content: This section contains two religious poems written by Sh. Abdalla al-Husniy, a famous religious scholar at the Hanisa Mosque in Mjua Kale, Mombasa. The poems were collected by Yahya Ali Omar, who was Sh. Abdalla's pupil, at the time of their composition in 1948 in Mombasa. The content is a religious admonition to instruct the Muslim community on how to abide by the Islamic values and duties and not to follow any forbidden activities. Sh. Abdalla was very famous for composing Waadhi at the time of the Maulidi celebration that he used to organise at the Anisa Mosque. The Maulidi celebration at the Anisa Mosque was very famous across East Africa.
General Note:
Al-Husniy, Abdalla, Sheik = Sh. Abdalla al-Husniy
Funding:
Digitised with funding from the Leverhulme Trust.

Record Information

Source Institution:
SOAS, University of London
Holding Location:
Archives and Special Collections
Rights Management:
This item is in the public domain. Please use in accord with Creative Commons license: Attribution-NonCommercial-ShareAlike (CC BY-NC-SA). High resolution digital master available from SOAS, University of London - the Digital Library Project Office.
Resource Identifier:
MS 380766a ( soas manuscript number )

Downloads

This item has the following downloads:


Full Text
140
P.J.L FRANKL & YAHYA AU OMAR
Shaykh Abd Allah died in Mombasa in 1375 AH/AD 1955, and
was buried outside the Anisa mosque the mosque \vith which his
name had been associated for so many years and where he now
'waits for the opening of the great Doomsday Book, in which nothing
is recorded of men but whether they meant good or evil, whether they
loved or neglected God'.
During his lifetime Mombasa was still recognisable as a Swahili,
Islamic town; but changes were already afoot which would efface the
Swahili character of Mombasa for all time.
MASHAIRI YA WAADHI
1 Bismillaki naama * jina la Mola muweza
nipate kuyatimiza * haya nalokusudiya.
2 kuusiya moyo wangu * na alo swahibu yangu
na Isilamu wenzangu * akubaliye wasiya.
3 Natuzidi kufikiri * tuzangaliye khatari
hakika zimekithiri * zimezidi kueneya.
4 Tangu zikiwa kwa siri * hata sasa ni dhahiri
imekuwa ni fakhari * kuyapanda maaswiya.
5 Zamani zimegeuka * mambo yameharibika
maovu yametukuka * hakuna wa kukemeya.
6 Tumeidharau dini * pasi na kuithamini
tumemtwii shetwani * hatuna kuzingatiya.
7 Na swala tumeziwata * misikiti twaipita
kwa ngoma na tarumbeta * wala hatuoni haya.
8 Imekuwa Ramadhani * ukenda migahawani
ni paziya milangoni * ndani wat 'u wajiliya.
9 Wangapi walo weza * wa zaka kuitimiza
na kwenda Maka waweza * hawatendi hata moya.
10 Twazini pasi na khofu * na kisha tukajisifu
na mengineyo machafu * siwezi kuwatajiya.


MASHAIRI YA WAADHl "VERSES OFADMONITION"
11 Na riba ndiyo amali * na kugema tembo kali
na yot'e twataka mali * ingawa twaangamiya.
12 Tumekuwa Isilamu * hatuchi tena haramu
twaiba tukidhilimu * na urongo kutumiya.
13 Kiburi ndiyo uvazi * kusengenya ndiyo kazi
na salata na upuzi * na kuyawata ya ndiya.
14 Wanawake nyuso wazi * watembeya wazi wazi
banati na vijakazi * wamekuwa hali moya.
15 Na twaa hakuna tena * ya wazee kwa vijana
wake wamekatazana * kutwii waume piya.
16 Na ndugu hawapendani * hakuna tena imani
na haki za majirani * zimetupwa zot'e piya.
17 Isilamu tumeswiri * kuigiza makafiri
kwa dhahiri na kwa siri * na dini kuitukiya.
18 Na mengineyo maovu * yaliyo na upotevu
tumeyashika kwa nguvu * pasi nyuma kurejeya.
19 Na yot'e twalohisabu * amekataza Wahabu
ameweka na adhabu * ya mwenye kuyangiliya.
20 Ukorofi duniyani * wa riziki na wa deni
na ikabu kaburini * na motoni kuingiya.
21 Na baa nyingi daima * za duniya na kiyama
na kuikosa salama * na mema kukwepukiya.
22 Na Mngu kughadhibika * na Mtume kuudkika.
na shufaa kukwepuka * hapo ndipo pa kuliya.
23 Ituze akili yako * ufikiri rnwisho wako
siku ya kutoka kwako * na wat 'u wakuliliya.


P.J.L FRANKL & YAHYA ALI OMAR
24 Huyu aliya mwanangu na mwengine ndugu yangu
mwana aliya babaangu nani uletuatiya.
25 Na mke awe mjani yupekee kit'andani
na vijana masikini hawana wa kuwaleya.
26 Uwate wat'u wako na yot'e majambo yako
na wot'e swahibu zako huzuni zimewangiya.
27 Vit'anda vyot'e na viti uepushwe kuvik'eti
wende ukalazwe nt'i * na sanda kukutatiya.
28 Ufukiwe kaburini wat'u warudi nyumbani
khofu nyingi na huzuni zot 'e zimekuskukiya.
29 Yak'oboke mato yako lipasuke tumbo lako
uwoze muili wako * mabuu wakijiliya.
30 Uwapi uzuri wako ziwapi jeuri zako
wawapi na wat'u wako yot'e yamekupoteya.
31 Kuna na kufufuliwa kaburini kutolewa
na moto kuutambuwa na swirati ndiyo ndiya.
32 Siku hiyo ifikiri ilo na nyingi khatari
na Hakimu ni Kahari hakuna kupendeleya.
33 Upawe hisabu yako uzione dhambi zako
uvikat'e vyanda vyako kuuma na kujutiya.
34 Na hayo hayako mbali yakaribu kweli kweli
itafakari ajali ghafula hukujiliya.
35 Ewe fakiri dhalili
36 ni lipi nambiya kweli Wallahi nakuapiya huna la kukuombeya
labuda ukitubiya * kwa Mola ukarejeya.


MASHAIRI YA WAADHI "VERSES OF ADMONITION"
37 Ujitahudi kukidhi * zilokufutu faradhi
uushike na waadhi * maisha kuutumiya.
38 Kulla wakati ujute * na maovu uyawate
na mema yasikupite * umuandame Nabiya.
39 Na ilimu ukisoma * uk'eti na wat'u wema
waovu wakikwegema * uwe mwenye kukimbiya.
40 Hifadhi viungo vyako * visimuasi Bwanako
umtwii Mola wako * kwa kulla alokwambiya.
41 Na haya ukiyashika utashukuru hakika
moto utakuepuka * na p'eponi utangiya.
42 Ya Rabbi tupe salama * duniyani na kiyama
utupe na mambo mema * maovu kutwepushiya.
43 Na swala ifikilize * na salamu iyeneze
kwa Mtume na Alize * daima kuwashukiya.
Mambasa 1368/1948 Abdallah Muhammad al-Husni
An English translatior
1 In the Name of God I begin
in the Name of the Almighty
so that I can accomplish
my intentions.
2 To give instruction to my heart
and to the one who is my close friend
and to my fellow Muslims
to (any) one who is ready to take advice.
3 Let us think hard
let us look at these dangers
truly they have multiplied
they have spread far and wide.


154
P.J.L. FRANKL & YAHYA ALI OMAR
STANZA 38
This stanza contains a minor technical blemish in that the final consonant
of la and lb is an unaspirated dental 't', while in 1c it is an unaspirated alveolar 't'.
STANZA 43
1a swala: mercy (i.e. rehema); if swala emanates from God (as it does in
this line) it carries this meaning, but if swala derives from Man then it denotes
'prayer(s)', as in Stanza 7.
2a alize: a contraction of aali zake 'his relatives'.

APPENDIX
WAADHI KWA MASHAIRI
1 Kwa jina la Mola wetu * twaanza maneno yetu
na swifa za Bwana wetu * na kuswaliya Nabiya.
2 Mwana adamu sikiya * yataka kuzingatiya
ina ghururi duniya * tahadhari nakwambiya.
3 Sighurike kwa ujana * wala kwa mali na wana
wala kwa wako ungwana * fahamu utapoteya.
4 Wat'u wot'e na majini * hangewaumba Manani
ela sahabu ya dini * yafahamu sana haya.
5 Shikamana na ibada * uifanye ndiyo ada
utaepukwa na shida * na kheri kukujiliya.
6 Na swala usiiwate * kipindi kisikupite
kwa nguzo na suna zot'e * na sharuti kuzitiya.
7 Mwenye kuwata kuswali * huwa kafiri wa kweli
kwa hadithi ya Rasuli * sikiya tena sikiya.
8 Kisha utowe na zaka * wende ukahiji Maka
na haya ukiyashika motoni hutangiya.
9 Ufunge na Ramadhani * kama ilivyo vyuwoni
sitezeteze na dini * fahamu utaangamiya
10 Na kujifunza ilimu ni wajibu Isilamu
mume na mke fahamu * ujinga una udhiya.
11 Usipojuwa ilimu * ibada haitotimu
fahamu kisha fahamu * khatarini utangiya.
12 Watwii wazee wako * wapende jirani zako
na Isilamu wenzako tahadhari kutukiya.
13 Usidhilimu chochot'e usisengenye yoyot'e
na zina nayo iwate * ukiyataka ya ndiya.


MASHAIRI YA WAADHI "VERSES OF ADMONITION" 155
14 Zingatiya mwanzo wako * na nguvu za Mola wako
matumboni mwa mamako * riziki kukungiliya.
15 Mekuleya matumboni * mezi tisiya yakini
huoni huonekani * wangojewa kutokeya.
16 Kisha kakuonya ndiya * yenye dhiki na udhiya
yako wewe kutokeya * duniyani kakutiya.
17 Ukitoka matumboni * uchafu mwingi mwilini
udhaifu masikini * huwezi ela kuliya.
18 Akawatiya huruma * wazee baba na mama
hata ukiwa yatima * hukosi wa kukuleya.
19 Tangu huwezi kusema * huwezi na kusimama
hata t'ungu kikuuma * huwezi kujiteteya.
20 Akakuumba kwa umbo * wallahi halina k 'ombo
akakupa mengi mambo * yakutengeza duniya.
21 La kwanza mato mawili * waona hapa na mbali
na mashikiyo mawili * kulla jambo wasikiya.
22 Mikono ya kushikiya * maguu ya kwendeya
ulimi wa kusemeya * na mdomo wa kuliya.
23 Tena amekupa p'uwa * harufu waitambuwa
na meno ya sawa sawa * vigumu watafuniya.
24 Amekupa na akili * mizani ilyo adili
la urongo na la kweli * waweza kutambuliya.
25 Na afiya na hifadhi * na kukupoza maradhi
sikiya wangu waadhi * udhibiti yot'e haya.
26 Neema nyingi ajabu * alizokupa Wahabu
huwezi kuzihisabu * wallahi nakuapiya.
27 Na zot'e hizo neema * kushukuru ni lazima
jaza ya mema ni mema * maovu kutoyatiya.
28 Mbona umeghafilika * kwa neno lisilo shaka
shetwani umemshika * umemuwata Nabiya.
29 Umejifanya mtesi * kwa Mola wako mkwasi
umevitupa viyasi * sina la kukwambiya.
30 Silaha zot'e ni zake * waila riziki yake
wayanwa na maji yake mbona umekosa haya?
31 Na vita vyako fahamu havimdhuru Karimu
ela wewe bahaimu * jijuwe utaumiya.
32 yatafakari mauti * yoyot'e hayamuati
wala hayana wakati * ghafula hukujiliya.
33 Ituze yako fikira * uwafikiri mabora
wenye ngome na minara na p'anga za kutindiya.


156 P.J.L. FRANKL & YAHYA ALI OMAR
34 Wawapi maFirauni * tena yuwapi Karuni
na Shadadi maliuni * wot'e wameangamiya.
35 Ajali zilipokwisa * Ziraili kawapesa
wakayawata mapesa * na mabo haya na haya.
36 Wameshukiya akhera * madhalili mafukara
uwapi wao ubora * yot'e yamewapoteya.
37 Wametoka duniyani * kwa viliyo na huzuni
wametiwa kaburini * sanda ubao mmoya.
38 Kaburi zimewakaza * hapana la kupumbaza
kot'e kumefunga kiza * adhabu huwashukiya.
39 Tena watafufuliwa * kiyama kuhisabiwa
Kisha wataaziriwa * mbele za Mitume piya.
40 Adhabu hizo ni k'uu * tena na moto kwa juu
majuto ni mjukuu * tahadhari na duniya.
41 Wapite na swiratini * waangukiye motoni
wateketee maini * maisha kuteketeya.
42 Na yot'e tuliyosema * yatakupata lazima
safari mbele na nyuma * wengine hutanguliya.
43 Na utakapo salama * ya duniya na kiyama
upate na mambo mema * yaepuke maasiya.
44 Fanya ibada kwa nguvu * usiwe mtepetevu
na kulla mt'u muovu * mwepuke hatuwa miya.
45 Uwombe na maghufira * na toba mara kwa mara
natuombe na sitara * Mngu tatukubaliya.
46 Atupe na taufiki * tuandame yalo haki
atupe nyingi riziki * na baa kutwepushiya.
47 Atupe nyingi amani * akhera na duniyani
atutie na p'eponi * motoni kutongiya.
48 Wot'e walohudhuriya * maulidi ya Nabiya
Mola tatutengezeya * kulla lilo na udhiya.
49 Atutiliye baraka * mak'ulima kulla mwaka
atuondolee na chaka * atupe na kheri piya.
50 Kulla aliye mjani * apate mwinyi imani
na vijana majumbani * wake wakituvyaliya.
51 Thuma swala na salamu * zimshukiye hashimu
na swahabaze kiramu * na ali na sisi piya.
Mambasa * Abdallah Muhammad al-Husni


Waadhi wa Sh. Abdalla al-Husniy

Item Reference: MS 380766a
Collection: Yahya Ali Omar Collection
File Reference: MS 380766
Title: Waadhi wa Sh. Abdalla al-Husniy
First lines of manuscript: Bismillahi naanza jina la Mola muweza nipate kuyatimiza haya nalokusudiya
Authors: Sh. Abdalla al-Husniy
Scribe:
AD Date: 1948
AD date of composition: 1948
AH Date: 1368
AH date of composition: 1368
Extent: 7 leaves
Resource Type: Poem
Poetic Form: Shairi
Format: Typescript
Language: Swahili
Script: Roman
Relevant Dialects: KiMvita
Subject and keywords: Swahili poetry, Islam, religious beliefs
People:
Biographical history: Sh. Abdalla al-Husniy was born in Mombasa at the beginning of 1900 in a family that originated from Hadramaut. He studied Islamic teaching with Sh. Said bin Ahmed, a well-known religious scholar. Sh. Abdalla became a Sheikh at the Anisa Mosque where he tought for many years and where he was buried in 1955. He was known for organising the Maulidi celebration, in the Anisa mosque, that was attended by many people from the Coast. After the maulidi he used to composed his famous waadhi, of which this one is an example. Sh. Abdalla was Yahya Ali Omar's religious teacher.
Archival history: Donated by Yahya Ali Omar in 2003
Physical characteristics: typescript in black ink
Electronic reproductions: None
Existence/location of copies: None
Finding aids: None
Relevant publications: P.J.L Frankl & Yahya Ali Omar. 19..Mashairi ya Waadhi. in AAP-Swahili Forum, Koln, Germany.
Notes:
Scope and content: This section contains two religious poems written by Sh. Abdalla al-Husniy, a famous religious scholar at the Hanisa Mosque in Mjua Kale, Mombasa. The poems were collected by Yahya Ali Omar, who was Sh. Abdalla's pupil, at the time of their composition in 1948 in Mombasa. The content is a religious admonition to instruct the Muslim community on how to abide by the Islamic values and duties and not to follow any forbidden activities. Sh. Abdalla was very famous for composing Waadhi at the time of the Maulidi celebration that he used to organise at the Anisa Mosque. The Maulidi celebration at the Anisa Mosque was very famous across East Africa.
Description
Location: None
Places: Mombasa


Full Text